Kijiji kilichoko kusini magharibi mwa Niger chashambuliwa watu 19 wauawa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 23, 2021

Usiku wa tarehe 21, wizara ya mambo ya ndani ya Niger ilitoa taarifa ikisema kwamba, kijiji kimoja kilichoko kusini magharibi mwa nchi hii kilishambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana, ambapo watu 19 waliuawa .

Taarifa hii ilisema, usiku wa tarehe 20, kikundi cha watu wenye silaha wasiojulikana waliingia kijiji cha mkoa wa Tillabéry, na wakawashambulia wanakijiji waliofanya ibada, ambapo watu 19 waliuawa na wengine 2 walijeruhiwa.

Wizara ya mambo ya ndani ya Niger imeimarisha hatua ya ulinzi kwenye eneo lililoshambulizwa, na inawasaka watu wenye silaha.

Mkoa wa Tillabéry uko mpaka kati ya Niger, Mali na Burkina Faso. Miaka hii ya karibuni, vikundi vyenye siasa kali na vikundi vya kigaidi vilivyohusika na kundi la ISIS vilifanya mashambulizi mara kwa mara kwenye eneo hilo, na kusababisha vifo na majeruhi vya watu wengi .

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha