Rais mpya wa Zambia ameapishwa kwenye sherehe kubwa ya kufurahisha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2021
Rais mpya wa Zambia ameapishwa kwenye sherehe kubwa ya kufurahisha
Agosti 24,2021, Hakainde Hichilema aliwapungia mkono waungaji mkono wake kwenye sherehe ya kuapishwa.
(Picha ilipigwa na Martin Mbangweta/Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua)

Mamia ya maofisa wa kisiasa na maelfu ya raia walikusanyika kwenye Uwanja wa mashujaa wa taifa huko Lusaka, Zambia wakishuhudia sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Hakainde Hichilema.

Ili kupata nafasi zao, mapema ya saa kumi ya asubuhi watu walikuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa michezo wakivaa fulana na kofia nyekundu ambayo ni rangi ya alama ya Chama cha Muungano wa Maendeleo ya Taifa, na sherehe hiyo ilipangiwa kufanyika saa tano asubuhi.

Hichilema alitoa hotuba baada ya kuapishwa, akisema, serikali yake itafanya juhudi kwa ajili ya maslahi ya raia wote, itarekebisha na kukuza uchumi ili kuwasaidia watu kuondoka na umaskini, itajitahidi kutimiza ahadi ilizotoa wakati wa kampeni, itajitahidi kurudisha utekelezaji wa sheria na heshima ya watu. Alisema: “Mnatukabidhi madaraka ya kusimamia mambo ya nchi hii, na tutakuwa watumishi wenu.”

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha