Algeria yatangaza kukatisha uhusiano wa kibalozi na Moroko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2021

Tarehe 24, waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Lamamra alisema, Algeria imeamua kukatisha uhusiano wa kibalozi na Moroko kuanzia siku hiyo.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku hiyo huko Algiers, mji mkuu wa Algeria, Bw. Lamamra alisema kutokana na “sera ya uhasama” dhidi ya Algeria iliyotekelezwa na Moroko kwa muda mrefu, serikali ya Algeria iliamua kukatisha uhusiano wa kibalozi na Moroko.

Bw. Lamamra alisema, maofisa wa Moroko walioko kwenye Umoja wa Mataifa walichochea mgongano kwenye uhusiano kati ya makabila madogo ya Algeria na serikali ya Algeria, na kupeleka uhasama wa nchi hizi mbili ufikie kileleni, kwa hiyo ni lazima serikali ya Algeria itoe jibu lake hili.

Mpaka sasa, serikali ya Moroko bado haijasema chochote kuhusu Algeria kutangaza kukatisha uhusiano wa kibalozi kati yake na Moroko.

Katika muda mrefu uliopita, kutokana na tatizo la Sahara Magharibi, uhusiano kati ya Moroko na Algeria umekuwa na hali ya wasiwasi, siku zote mpaka kati ya nchi hizi mbili unafungwa. Tarehe 18, Agosti, mwaka huu, rais Tebboune wa Algeria aliwahi kusema kwenye mkutano kuhusu usalama kuwa, kutokana na Moroko iliongeza “vitendo vya uhasama” dhidi ya Algeria, Algeria inalazimika kufikiria tena uhusiao kati ya nchi hizi mbili.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha