Uganda yaanza kugawa chanjo za Sinovac zilizozawadiwa na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 27, 2021
Uganda yaanza kugawa chanjo za Sinovac zilizozawadiwa na China
(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Duka la Matibabu la Kitaifa la Uganda (NMS) lilisema jumatano hii kuwa, chanjo laki tatu za Covid-19 za Sinovac zilizozawadiwa na serikali ya China zimeanza kugawanywa kwa sehemu mbalimbali nchini Uganda.

Nchi hiyo inalenga kuwadunga watu milioni 22 au nusu ya idadi ya watu wake wote ili kuzuia maambukizi ya Corona.

Tangu ilipoanzisha udungaji wa chanjo mwezi wa tatu mwaka huu hadi jumanne hii, watu milioni 1.2 hivi wamedungwa na chanjo za Corona.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha