Umoja wa Afrika wakabidhiwa chanjo za COVID-19 za China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2021
Umoja wa Afrika wakabidhiwa chanjo za COVID-19 za China
(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Alhamisi wiki iliyopita, Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) ilikabidhiwa chanjo za COVID-19 kutoka China huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

Kaimu mwakilishi wa China aliyeko Umoja wa Afrika Chen Xufeng alisema kwenye hafla ya kukabidhi chanjo kuwa, "Chanjo hizo zilizozawadiwa na serikali ya China zitatumiwa kwa wawakilishi wa AU na nchi za Afrika walioko huko Addis Ababa."

Bw. Chen alisisitiza, tangu Corona ilipoanza kuambukiza, China imeitolea Afrika vitu vinavyohitajika kwa dharura pamoja na mamilioni ya chanjo. "Siku zote China inazipa kipaumbele nchi za Afrika katika utoaji wa chanjo." Na pia Bw. Chen aliongeza kuwa hadi sasa China imetoa chanjo kwa nchi na mashirika 47 ya Afrika.

Kamishna Bw. Bankole Adeoye wa AU anayeshughulikia mambo ya kisiasa, amani na usalama aliisifu China kwa msaada wake uliotolewa kwa wakati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha