Kenya itakusanya dola ya Marekani laki 9.1 kuwalinda tembo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2021

Jumatatu ofisa mwandamizi wa serikali ya Kenya alisema, Kenya itakusanya shilingi milioni 100 (sawa na dola ya Marekani laki 9.1) zitakazotumiwa kuwalinda tembo, ambao ni alama ya wanyamapori .

Najib Balala, sekretari wa Baraza la Mawaziri la utalii na wanyamapori alisema, pesa hizo zitakusanywa kutoka michango itakayotolewa katika siku ya Kenya ya kuwapa tembo jina.

Pesa zinazokusanywa zitatumiwa pia kudumisha utekelezaji wa mpango wa kuwalinda tembo, ambao unalenga kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori wakiwemo mamalia wakubwa. Balala aliongeza kuwa, nchi hii ya Afrika Mashariki ilipoteza tembo 386 mwaka 2013, lakini mwaka 2020, tembo waliopotezwa walikuwa 11. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha