Ndege tatu za kivita za Russia zafuata ndege ya upigaji mabomu ya Marekani kwenye anga juu ya bahari ya Okhotsk

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 27, 2021

Tarehe 26, Makao makuu ya ulinzi wa taifa wa wizara ya ulinzi ya taifa ya Russia yalisema kwamba, ndege 3 za kivita za Russia-35s ziliruka angani kwa dharura siku hiyo, zikifuata ndege ya upigaji mabomu ya kimkakati ya jeshi la anga la Marekani B-52H, ambayo ilikuwa imekaribia mpaka wa anga ya Russia kwenye anga juu ya bahari ya Okhotsk ya Mashariki ya mbali.

Makao makuu hayo yalisema, tarehe 26, saa 1 jioni ya saa za huko, rada ya ulinzi wa anga ya eneo la kijeshi la mashariki ya Russia iligundua kitu kimoja kwenye anga juu ya bahari ya Okhotsk ambacho kilikuwa kinakaribia mpaka wa Russia. Ndege 3 za kivita za Russia-35s ziliruka angani kwa dharura, na kutambua kitu kile ni ndege ya upigaji mabomu ya kimkakati ya jeshi la anga la Marekani B-52H, na zikaifuata. Halafu ndege hiyo ya upigaji mabomu ya Marekani iliondoka kutoka mpaka wa Russia, na ndege za Russia zilirudi salama kwenye uwanja wa ndege wa kituo chao.

Makao makuu hayo yalisema, katika muda wote wa urukaji, ndege za Russia zilikuwa zinafuata kwa umakini kanuni za matumizi ya eneo la anga la kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha