Ukuta wa Mji wa Xi’an: Ukale unapokutana na Usasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2021

Ukuta wa Mji wa Xi'an ni ukuta wa mji wa zamani zaidi na uliohifadhiwa sana nchini China na pia kivutio cha utalii wa saini katika Xi'an, mji mkuu wa Mkoa wa China wa Shaanxi unaopatikana Kaskazini Magharibi mwa China.

Watu wengi wanaweza kushangaa, kuwepo kwa pamoja urithi wa utamaduni na kivutio cha utalii, namna kuta za mji zinaweza kuweka mizania kati ya uhifadhi na ustawi.

Wu Chun, Mkurugenzi Msaidizi wa kamati ya menejimenti ya Ukuta wa mji wa Xi'an, anaelezea juhudi ambazo zimefanywa kulinda muundo wa kale. Wameimarisha timu ya kitaalamu kwa ajili ya uhifadhi na urejeshaji wa ukuta baada ya juhudi za miaka 20. Timu hii haijaweka mkazo pekee katika kulinda muonekano wa ukuta bali pia katika kuchanganya muundo wa kuta hizi kuleta maendeleo ya kisasa ya Xi'an, zaidi kuufufua ukuta na kuufanya kuwa na muonekano mpya na mvuto.

Ufuatililaji madhubuti kuhakikisha usalama wa Ukuta

Ukuta wa Xi'an, ukiwa na mzunguko wa kilomita 13.74, unahusisha vifaa kadhaa vya ulinzi wa kijeshi, ukiwa umeendelezwa kuwa alama kuu ya mjii huu wa kimataifa ambao ni tajiri wa historia na utamaduni.

Majengo haya ya kiasili muda wote huwa na shughuli mbalimbali zinaendelea. Watembeleaji wanaweza kupanda kuta na hupewa zawadi ya picha ya mandhari ya mji huo huku wakifurahia maonesho ya mwanga ambayo huoneshwa kwenye kuta, kuendesha baiskeli au kukimbia mbio za masafa marefu pembezeni mwa mzunguko wa kuta. Watu wengi wanashangaa ni kwa namna gani miundombinu hiyo ya kale inaweza kudumu kwa miaka mingi? Namna gani ukuta umekuwa ukihifadhiwa muda wote huu?

Changamoto nyingi zilijitokeza wakati mji ukijaribu kurejesha sifa ya zamani ya ukuta na kuubadili kuwa kivutio cha kitalii. Kwahiyo, kamati ya menejimenti imepata mafunzo kutoka kwa changamoto hizo katika kusimamia masuala ya urithi wa utamaduni ndani na nje, na baada ya juhudi za miaka, mfumo rasmi wa menejimenti umeimarishwa katika jitihada za kuulinda kisayansi ukuta wa mji.

Wu alisema kwamba zaidi ya vituo 8,000 vya ufuatiliaji ukuta vimeanzishwa, ambavyo vinazunguka kuta za mji, majengo ya kale, mikondo ya maji inayozunguka kuta, treni ndogo za umeme (subways) na pia shughuli za kitalii. Kulingana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwenye vituo hivi vya ufuatiliaji usimamizi wa kuta, hatua nne za kutoa taarifa za awali za tahadhari zimeanzishwa ili kusaidia kazi ya ufuatiliaji. Hivyo, kwa kufuata hatua tofauti za tahadhari, mfumo udhibiti athari kabla hazijatokea na mipango ya dharula inaweza kuchukuliwa kila tatizo linapojitokeza

Hatua mbalimbali kufufua kuta zikiwa na usasa

Si muda mrefu uliopita, Ukuta wa Mji wa Xi’an uliandaa onesho la kuvutia la mwanga kusheherekea sikukuu ya katikati ya mwezi. Onesho hili lilitoa rangi ya kuvutia kutoka kwenye mji wa kale.

Katika miaka ya hivi karibuni, ukiachilia mbali uhifadhi wa urithi wa utamaduni na masalia ya kale, kivutio hiki cha utalii kimeweka juhudi katika kuendeleza utamaduni wa asili ya China na kuupa utamaduni wa kale uhai mpya katika mazingira ya kisasa.

Kwa mujibu wa Wu, kuna maonesho mawili ya mwanga ambayo huoneshwa kwenye kona ya mnara wa Kusini-Mashariki mwa ukuta na Kusini-Magharibi sawia. Moja linamuonesha ‘shujaa wa ukuta wa mji’, uhusika wa pekee ambao umebuniwa kuwasilisha historia ya kale, kufuata maisha ya furaha, ukataji wa karatasi wa asili na maonesho 24 yanayoonesha urithi wa taifa kutoka makumbusho ya kihistoria ya Shaanxi. Watalii na wenyeji wanaweza kufurahia shamrashamra za maonesho kwa macho yao na kupata ufahamu kuhusu utamaduni wa jadi wa kichina.

Kamati ya menejimenti ya ukuta wa Xi’an imetumia rasilimali za utalii kikamilifu na kuanzisha shughuli mbalimbali za kiutamaduni na kisanaa ambazo zinavutia idadi kubwa ya watalii kutoka karibu na mbali kutazama. Kwa kuangaza siku zijazo, ukuta huu wa mji wa Xi’an unatazamia kuboreshwa kuwa kivutio bora cha Dunia kikihusisha ulinzi wa urithi, maonesho ya kitamaduni, utazamaji mandhari, maeneo ya kielimu na burudani. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha