Kikosi cha matibabu cha Jeshi la kulinda amani la China nchini Congo-Kinshasa chakabidhi kazi kwa duru ya 24

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2021
Kikosi cha matibabu cha Jeshi la kulinda amani la China nchini Congo-Kinshasa chakabidhi kazi kwa duru ya 24

Mchana wa Tarehe 27, Septemba, katika hospitali ya ngazi ya pili ya China ya ujumbe maalumu wa kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Congo-Kinshasa, kikosi cha 24 na cha 25 cha jeshi la kulinda amani la China katika nchi hiyo vimefanya “hafla ya kukabidhi kazi ya duru ya 24”. Hafla hiyo inamaanisha kikosi cha 25 cha jeshi la kulinda amani kimeanza kutekeleza kazi yake nchini Congo-Kinshasa.

Katika mwaka mmoja uliopita, kikosi cha matibabu cha 24 cha jeshi la kulinda amani kilishinda taabu nyingi katika hali ya maambukizi ya Corona. Kwa ujumla waliwatibu wagonjwa zaidi ya 600 na kufanya upasuaji zaidi ya 230. Mwezi Julai mwaka huu, askari 43 wa kikosi hicho cha jeshi la kulinda amani wote walitunukiwa “nishani ya amani” na Umoja wa Mataifa. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha