Waziri Mkuu wa China asisitiza upatikanaji wa utulivu wa nishati, na usalama wa nishati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2021
Waziri Mkuu wa China asisitiza upatikanaji wa utulivu wa nishati, na usalama wa nishati
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, mjumbe wa kudumu wa ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya nishati, akiongoza kikao cha Kamati ya Kitaifa ya nishati kilichofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, tarehe 9 Oktoba, 2021. Naibu Waziri Mkuu wa China Han Zheng, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Naibu Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya nishati, pia alihudhuria kikao hicho. (Xinhua / Ding Haitao)

BEIJING, (Xinhua) - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amesisitiza uwepo wa uhakika wa upatikanaji wa nishati ili kusaidia kuongeza maendeleo yasiyoleta uchafuzi.

Li, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Kamati ya Kudumu ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Nishati, amesema katika mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki kwamba, nchi hiyo inapaswa kusawazisha maendeleo na utoaji wa kaboni, kuzidisha mageuzi ya sekta ya nishati , na kuongeza mageuzi sekta hiyo kuwa sekta isiyotoa uchafuzi. Usalama wa nishati huhusisha usalama wa maendeleo na usalama wa taifa, Li alibainisha, akisisitiza mahitaji ya nchi kujenga mfumo wa kisasa wa nishati kwa msingi wa kuhakikisha upatikanaji wa nishati na kuweka mkazo katika kuongeza uwezo wa utoaji wa nishati.

Li Keqiang amesema, lengo la China la kufikia kilele cha utoaji wa kaboni ifikapo mwaka 2030 na kufikia kiwango cha kusawazisha Carbon ifikapo mwaka 2060 linaendana na mahitaji yake ya mageuzi ya uchumi na mahitaji ya kushirikiana kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Li ametaka juhudi za kuhakikisha uthabiti kwenye mnyororo wa uzalishaji na usambazaji na kuendeleza uchumi kwa utulivu. Juhudi hizi lazima ziongezwe kipindi hiki cha kukuza matumizi ya nishati safi, kuongeza uwiano wa matumizi ya jumla ya nishati safi, na maendeleo ya yasiyoleta uchafuzi.

Li pia amesisitiza juhudi za kuimarisha utafiti na maendeleo katika teknolojia za nishati safi na kutoa carbon kwa kiwango cha chini, kuboresha kiwango cha ufanisi wa gridi ya umeme, na kupunguza matumizi ya nishati na utoaji wa Carbon kwa kutegemea mifumo ya soko.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha