Somalia yakataa pendekezo la AU la kikosi cha mseto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 14, 2021

MOGADISHU - Serikali ya Somalia imekataa pendekezo la Umoja wa Afrika (AU) la kuunda kikosi cha mseto na Umoja wa Mataifa (UN) ili kulinda amani nchini humo.

Serikali ya Somalia Jumanne ya wiki hii imesema Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AUPSC) halikuzingatia maoni ya Somalia, pamoja na kuunda timu ya pamoja ya kiufundi itakayotathmini njia nzuri kwa nchi hiyo.

Somalia imesema inakataa kwa nguvu zote pendekezo hilo, kwamba Umoja wa Afrika unapaswa kushikilia mpango wake wa awali chini ya Mpango wa Mpito wa Somalia, badala ya kupitisha mpango wa kulinda amani nchini Somalia wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

 "Serikali ya Somalia inaeleza wasiwasi mkubwa kutokana na AUPSC kuendelea kupuuza mamlaka ya Somalia, kutoheshimu ukamilifu wa ardhi yake na uhuru wa kisiasa kwa kuendeleza ajenda ambayo inakiuka haki za kimsingi za nchi mwanachama," Wizara ya Ulinzi ya Somalia imesema katika taarifa iliyotolewa Mogadishu.

Chini ya Mpango wa Mpito wa Somalia, kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kina jukumu la kuhakikisha kwamba Jeshi la Polisi la Somalia lina uwezo wa kutosha wa kuchukua jukumu kamili la kudumisha sheria na utulivu nchini humo wakati AMISOM itakapoondoka mnamo Mwaka 2022.

Taarifa ya Wizara ya ulinzi ya Somalia imetolewa baada ya AUPSC kuidhinisha kuundwa kwa kikosi cha mseto cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa sehemu ya 7 yakatiba ya Umoja wa Mataifa, ambayo itahakikishia fedha za kutabirika na endelevu za miaka mingi kwa opereseheni za baadaye, kupitia michango itakayotathminiwa na Umoja huo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha