Ndoto ya pamoja ya China na Namibia yang’ara kwenye anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2021

(Picha inatoka www.cfp.cn)

Tarehe 17, Septemba, mwaka 2021, chombo cha Shenzhou No.12 cha kubeba binadamu kwenye safari ya anga ya juu kilirudi kwenye ardhi. Licha ya vifaa vya kawaida vya kufanya majaribio, chombo hicho pia kilibeba kitu kingine maalum yaani bendera ya taifa ya Namibia. Ndani ya miezi mitatu baada ya kurushwa kwa chombo cha Shenzhou No.12, bendera hii ilisafiri angani pamoja na wanaanga watatu wa China.

Ushirikiano wa safari kwenye anga ya juu kati ya China na Namibia ulianzia mwaka 2000. Mwaka mmoja baadaye, kituo cha kupima na kudhibiti hali ya safari ya chombo kwenye anga ya juu cha China kilizinduliwa kwenye kitongoji cha mji wa Swakopmund, Namibia. Katika miaka 20 iliyopita, kituo hicho kimeshuhudia matukio mengi makubwa yaliyofungua ukurasa mpya mmoja baada ya mwingine kwenye historia ya maendeleo ya chombo cha safari kwenye anga ya juu cha China, na pia kimekuwa kielelezo cha kuhuisha kwa amani mradi kwenye anga ya juu kwa nchi hizo mbili.

Katika miaka 20 iliyopita, kituo hicho kilitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Namibia kuhusu teknolojia ya safari kwenye anga ya juu, na kuisaidia Namibia kuwaandaa watu wengi wenye utaalam.

Mambo ya safari kwenye anga ya juu ya China si kama tu ni mambo ya China, bali pia ni mambo ya Afrika nzima na binadamu wote. Kwenye mchakato wa kujenga jumuiya ya maendeleo ya dunia nzima yenye mustakabali wa pamoja, hakika wafanyakazi wa safari ya anga ya juu wa China na Namibia wataweka nyayo zisizofuta daima kizazi baada ya kizazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha