Uendeshaji wa miaka 10 wa kituo cha vielelezo vya kilimo cha Rwanda kilichojengwa kwa msaada wa China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 18, 2021
Uendeshaji wa miaka 10 wa kituo cha vielelezo vya kilimo cha Rwanda kilichojengwa kwa msaada wa China
(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

"Nikiona tabasamu za wakulima na kusifiwa nao, naona nimepata mafanikio makubwa zaidi." Alipozungumia uyoga wa kula unaopandwa kwa teknolojia ya China unapendwa sana na Wanyarwanda, macho ya mtaalamu wa kilimo wa China Bw. Zhu Su yaling'aa.

Kituo cha vielelezo vya teknolojia ya kilimo cha Rwanda kilichojengwa kwa msaada wa China kiko kwenye Mji Huye na kilizinduliwa rasmi mwaka 2011. Mnamo mwaka 2012, Bw. Zhu Su alifika Rwanda akibeba jukumu la kufanya utafiti na kueneza upandaji wa uyoga wa kula. Tangu hapo alijikita katika kazi hiyo huko kwa miaka tisa.

Bw. Zhu Su alisema, "Tumewaandaa mafundi wa kilimo na wakulima wenye ujuzi zaidi ya 5000 nchini Rwanda. Hivi sasa uyoga wa kula ni shughuli muhimu katika uchumi wa nchi hiyo na ni mradi wake mkuu wa uenezaji."

Mfanyakazi wa kituo hicho alimwambia mwandishi wa habari kuwa, katika miaka minne tangu alipofanya kazi kwenye kituo hicho, mshahara wake uliongezeka kwa mara nne. "Hivi sasa sio vigumu kwangu kupata riziki za familia."

Mkurugeni wa Kamati ya Kilimo ya Rwanda Bw. Patrick Karangwa alisema, teknolojia ya upandaji wa uyoga wa kula imechangia kuongeza nafasi za ajira, kuhakikisha usalama wa chakula na kuongeza kipato, na imefanya kazi muhimu kwenye kutatua tatizo la utapiamlo la Wanyarwanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha