Ujumbe wa Syria kukutana huko Geneva kwa mazungumzo kuhusu katiba ya Syria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 18, 2021

GENEVA - Duru ya mpya ya mazungumzo kuhusu katiba ya Syria, yanayoshirikisha wajumbe wa chombo kidogo cha Kamati ya Katiba ya Syria, itaanza Geneva Jumatatu hii.

Mjumbe Maalum wa UN kuhusu suala la Syria Geir O. Pedersen amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari hapa Jumapili kwamba, pande zinazohusika na suala la Syria zimekubaliana kuandaa na kuanza kuandika rasimu ya mabadiliko ya katiba, na "jambo jipya wiki hii ni kwamba kwa kweli tutaanza mchakato wa kuandaa rasimu ya mabadiliko ya katiba ya Syria"

Mwakilishi huyo wa UN amesema kwamba Jumapili asubuhi, alikuwa amekutana na wenyekiti wa pamoja walioteuliwa na serikali ya Syria na upande wa upinzani.

"Kwa mara ya kwanza, Wenyekiti hao wawili, mmoja aliyeteuliwa na serikali na mwingine aliyeteuliwa na upinzani, walikuwa wamekaa pamoja nami kwa mazungumzo muhimu na ya utayari juu ya jinsi tutakavyoendelea na mabadiliko ya katiba na kwa kweli kwa kina jinsi tunavyojipanga kwa wiki iliyo mbele yetu, "Pedersen amesema.

Mjumbe huyo wa UN amewaambia waandishi wa habari kuwa hali ya kibinadamu na uchumi nchini Syria ni ngumu sana, akibainisha kuwa kuna zaidi ya Wasyria milioni 13 wanaohitaji msaada wa kibinadamu.

Kamati ya Katiba ya Syria - ambayo inajumuisha wawakilishi wa serikali ya Syria, upinzani, na jamii za kiraia - ilizinduliwa rasmi huko Geneva mnamo Oktoba 30, Mwaka 2019 kutunga katiba mpya ya nchi hiyo.

Chombo hicho kidogo cha Kamati ya kitaifa ya Katiba, kinaundwa na wajumbe 45 ambao wajumbe 15 kutoka kila upande, wamekutana huko Geneva mara tano, bila kufikia maendeleo yoyote makubwa. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha