Kikundi cha kupiga filamu ya anga ya juu cha Urusi charudi kwenye dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 19, 2021

Chombo cha “Soyuz” kilichobeba mwanaanga mmoja na wapiga filamu wawili kilirudi kwenye ardhi ya dunia tarehe 17. Wapiga filamu wawili walikaa kwenye kituo cha anga ya juu cha kimataifa kwa siku 12, ambapo walipiga filamu ya mada kuhusu anga ya juu.

Shirika la habari la Sputnik la Russia lilitoa habari zikisema, tarehe 17, saa moja na dakika 35 ya saa za Moscow (yaani tarehe 17, saa sita na dakika 35 ya saa za Beijing), chombo cha “Soyuz MS-18” kilichobeba mwigizaji Yulia Pelehild, mwongozaji Krim Shipenko na mwanaanga Oleg Nowitzki walipanda kilitua katika Kazakhstan baada ya kuruka kwa zaidi ya saa tatu.

“Kimetua! Karibuni nyumbani!” Idara ya usafiri wa anga ya juu ya Russia Roscosmos ilitoa habari kwenye mitandao ya kijamii ya Twitter, na kutangaza moja kwa moja mchakato wa kutua kwa chombo hicho na ilisema, watu hao watatu walihisi vizuri.

Idara ya usafiri wa anga ya juu ya Russia Roscosmos ilisema, lengo la kupiga filamu hiyo ni kuwavutia vijana wengi zaidi wafuatilie sekta ya usafiri kwenye anga ya juu.

(Liu Xi/ Shirika la Habari la China Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha