Makala: China inavyoongeza uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2021

Tunapozungumzia ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika, mara nyingi watu wanafikiria miradi mikubwa ya miundombinu kama ujenzi wa reli, mitambo ya umeme na migodi.

Lakini ukweli ni kwamba, kuongezeka kwa uhusiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hiyo barani Asia lenye nguvu zaidi za kiviwanda na nchi za Afrika, kumezifanya pande zote mbili kushuhudia kuongezeka kwa biashara na kubadilisha hali ya maisha ya watu.

Mwaka 2009 China iliipita Marekani na kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara barani Afrika na tangu wakati huo imesalia katika nafasi hiyo kwa miaka 12 mfululizo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Biashara ya China, biashara kati ya China na Afrika imeongezeka mara 20 katika miaka 20 iliyopita hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 180 Mwaka 2020, ikichukua asilimia 21 ya biashara yote ya nje ya bara hilo kwa mwaka ule.

Jumla ya thamani ya biashara kati ya China na nchi za Afrika imeongezeka kwa asilimia 40.5 na kufikia dola za kimarekani bilioni 139.1 katika kipindi cha miezi saba ya kwanza ya Mwaka 2021 licha ya kuendelea kuwepo kwa janga la UVIKO-19.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Baraza la Biashara kati ya China na Afrika inasema kuwa, Makampuni ya binafsi ya China, badala ya makampuni makubwa yanayomilikiwa na taifa, yamechukua nafasi kubwa zaidi katika kuhimiza ongezeko la kasi la ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika.

Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa kwenye Gazeti la China Daily, kutokana na ushirikiano wa kibiashara, China imechangia maisha bora kwa Waafrika kwa kuuza mashine yake kwa bei nafuu barani Afrika, ambazo zimeongeza uzalishaji na kuongeza mapato kwa wafanyakazi, na vilevile kutoa ajira nyingi, amesema Gitahi Ngunyi, mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Kenya.

Aidha, katika kipindi cha Januari hadi Julai, Mwaka 2021 kiwango cha bidhaa zilizoagizwa na China kutoka nchi mbalimbali za Afrika kimeongezeka kwa asilimia 46.3 na kufikia dola za kimarekani bilioni 59.3, huku uagizaji wa bidhaa za kilimo kama vile mpira, pamba na kahawa umeongezeka maradufu kuliko mwaka uliopita wakati kama huo.

Qian Keming, Naibu Waziri wa Biashara wa China, alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliohusu maandalizi ya Maonesho ya pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika, kwamba China inapanua zaidi uagizaji wa bidhaa zisizo za rasilimali au zilizosindikwa kutoka Afrika, hususani bidhaa zilizoongezewa thamani, huku Afrika inahimiza muundo wa uchumi anuwai kupitia shughuli kama usindikaji wa kina wa rasilimali zake na bidhaa za kilimo.

China inajitahidi kupunguza hali isiyo na uwiano ya biashara kati yake na Afrika, kwa kuagiza aina nyingi za bidhaa kutoka Afrika, amesema Jeremy Stevens, mchumi mkuu wa Benki ya Standard anayeshughulikia uchumi wa China, taasisi ya fedha yenye huduma za kifedha kwa nchi za Afrika, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Anaona kuwa wakati Afrika inataka kukuza sekta ya viwanda ili kuongeza ajira na kujenga muundo wake wa uchumi wa anuwai, China inataka kuwa mshirika ambaye anasaidia ukuaji na maendeleo ya Bara la Afrika. Hiyo inaonesha ushirikiano wa kweli.

"Kama China inauza bidhaa nyingi kwa nchi zote za Afrika na kununua malighafi chache kutoka nchi nne au tano za Afrika, itadhoofisha moyo wa ushirikiano huo," amesema.

Huku janga la UVIKO-19 bado halijadhibitiwa kote duniani, China na Afrika zimeonesha jinsi uhusiano wa pande mbili unavyoendelea kustawisha chini ya janga hilo.

Wakati janga la UVIKO-19 lilipoiathiri China na Wachina wanapopambana virusi hivyo, nchi za Afrika zilitoa msaada wa hali na mali kwa China.

Baada ya nchi hiyo kufanikiwa kudhibiti kikamilifu ugonjwa huo nchini, China pia ilionesha jinsi rafiki wa kuaminika anavyounga mkono juhudi za Afrika katika kupambana na janga hilo.

Nchi ya China imeendelea kutoa idadi kubwa ya vifaa vya matibabu vinavyohitajika barani Afrika na pia kutuma timu za wataalam wa matibabu.

Mbali na kuchangia chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa nchi za Afrika, China pia inaendelea kuisaidia Afrika katika kuzalisha chanjo hizo kwa kutoa teknolojia na ujuzi.

Kampuni ya dawa ya China Sinopharm imesema imekuwa ikitoa misaada ya matibabu na vifaa vya kupambana na janga hilo linalosababishwa na virusi vya korona kwa nchi 51 za Afrika. Idadi ya chanjo za China kwa nchi za Afrika imezidi dozi milioni 55.95. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha