Kifo cha Powell kilichotokana na matatizo ya UVIKO-19 chazusha mjadala wa ufanisi wa chanjo nchini Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2021
Kifo cha Powell kilichotokana na matatizo ya UVIKO-19 chazusha mjadala wa ufanisi wa chanjo nchini Marekani
Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Marekani Colin Powell akihudhuria Mkutano wa 2013 wa Baraza la Russia huko Moscow, Russia, Aprili 18, 2013. (Xinhua / Liu Hongxia)

Kufariki Dunia kwa Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Colin Powell kumeongeza mjadala mkali kwa wapinga chanjo dhidi ya UVIKO-19 nchini humo, lakini wataalam wa afya wamesisitiza kwamba kifo cha mwanadiplomasia huyo hakitokani na kupokea chanjo hiyo, si ushahidi kwamba chanjo hazifanyi kazi.

WASHINGTON - Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Colin Powell, juzi Jumatatu ameaga Dunia akiwa na umri wa miaka 84 kutokana na magonjwa yanayotokana na UVIKO-19, hivyo kusababisha mjadala mkali juu ya ufanisi wa chanjo nchini Marekani.

"Jenerali Colin L. Powell, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani na Mwenyekiti wa baraza la pamoja la Wakuu wa Jeshi, amefariki dunia asubuhi ya leo kutokana na magonjwa yanayosababishwa na UVIKO-19" familia ya Powell imeandika kwenye ukurasa wa Facebook Jumatatu ya wiki hii, ikisisitiza Powell alikuwa amepokea kikamilifu chanjo. Alikuwa akisumbuliwa na magonjwa mengine.

Kifo cha Powell kimezusha mjadala mkali miongoni mwa wapinga chanjo nchini Marekani lakini wataalam wa afya wamesisitiza kwamba kifo chake hakina uhusiano wowote na kinga ya chanjo, siyo ushahidi kuwa chanjo hazifanyi kazi.

"Pamoja na kuwa Powell alikuwa amepata chanjo kamili, pia alikuwa na saratani ya uboho wa mfupa, saratani ambayo inazuia kinga ya mwili" amesema Gwen Nichols, afisa mkuu wa matibabu katika Taasisi ya Kansa ya Damu ya Marekani.

"Kansa ya Multiple myeloma iliyosambaa mwilini haitibiki, kwa hivyo hata kama amepata matibabu au hakupata matibabu, ugonjwa wake na umri wake, vilimfanya awe katika hatari ya kuambukizwa, kusababisha magonjwa mengine na kufariki" ameeleza.

"Nina wasiwasi watu watasema chanjo haikumsaidia," Robert Murphy, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa afya wa kimataifa ya chuo cha matibabu cha Feinberg katika Chuo Kikuu cha Northwestern.

"Kifo cha Powell kinaashiria haja ya tahadhari katika vita vya Marekani dhidi ya virusi vya korona vya muda mrefu, ikionesha hatari inayoendelea ya janga hilo kwa maisha ya Wamarekani" inasomeka habari iliyochapishwa na gazeti la The Hill.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha