Kurejeshwa kwa Kiti halali cha China katika UM hatua muhimu kwa Dunia: Afisa wa UM

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2021

BEIJING - Siddharth Chatterjee, Mratibu Mkazi wa Mfumo wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini China, amesema, maadhimisho ya miaka 50 ya kurudishwa kwa kiti halali cha China katika Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu sana, sio kwa China tu, bali kwa dunia nzima.

"Ninapongeza China kwa mafanikio yaliyopatikana katika miaka 50 iliyopita," Chatterjee amesema katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua, akisifu mchango wa China "ikiwa mshiriki wa mfumo wenye pande nyingi ya Umoja wa Mataifa, na mhimizaji wa katika umoja huo. "

Huku akikumbusha historia, Chatterjee amesema kuwa, wakati UM ilipofungua ofisi yake kwa mara ya kwanza nchini China, ikitoa misaada, maarifa na uzoefu wa kupunguza umaskini, na kadhalika, China iliafikiana na yote.

Kwa maoni yake, China imefanya vema katika kushughulikia mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya binadamu na heshima, ikiwa ni pamoja na elimu, afya na kadhalika. Katika kipindi cha mpango wa 14 wa miaka mitano, China inalenga kupunguza ukosefu wa usawa, kuhakikisha mfumo mzima wa kijamii unaungana na malengo ya UM ya maendeleo endelevu.

Pamoja na kutambua mafanikio ya China ya kuwaondoa watu milioni 770 kutoka kwa umaskini katika miongo minne iliyopita, Chatterjee amesema kuwa "ni maarifa ambayo sisi, Umoja wa Mataifa, tunataka kushirikisha nchi zote zinazoendelea, na kwamba zinawezekana kufikia mafanikio hayo"

Aliongeza kuwa, mwaka huu ni muhimu, kwa kuwa ni mwaka wa 50 wa China kurudi katika kiti chake halali cha UM na pia ni miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na cha muhimu zaidi ni kwamba katika miaka tisa ijayo, UM inapaswa kuharakishakutimiza ajenda yake ya mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu.

Tarehe 25 Oktoba, Mwaka 1971, katika kikao chake cha 26, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio namba 2758 kwa kura nyingi za ndio. Azimio hilo liliamua kurejesha haki zote halali za Jamhuri ya Watu wa China katika UM na kuwatambua wawakilishi wa serikali yake kama wawakilishi halali na wa pekee wa China katika UM.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha