Wazazi kutoka Cameroon wamshukuru daktari wa upasuaji wa China kwa kuokoa maisha ya mtoto wao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 21, 2021

(Picha inatoka ChinaDaily.com.cn)

Daktari bingwa wa upasuaji wa neva wa Hospitali ya Watoto ya Wuhan Deng Wenyue na wenzake hivi karibuni wamepokea bango maalum la hariri likiwa na maandishi ya shukrani kwa lugha ya kiingereza kutoka kwa wanandoa wakielezea shukrani za dhati.

Bango hilo lilitolewa na Akinnet Akiy na mkewe Linnet Boh kwa kuishukuru timu ya matibabu baada ya binti yao wa miezi 6 Aubrey kuruhusiwa kutoka hospitalini mnamo Oktoba 11 mwaka huu kufuatia upasuaji wa dharura uliofanyika kwa mafanikio.

"Asante kwa daktari wa China. Tulipokea matibabu bora na ukarimu katika Hospitali ya watoto ya Wuhan. Ninamshukuru sana Daktari Deng kwa msaada wake. Urafiki wa China na Cameroon udumu milele" wanandoa hao waliandika kwenye bango hilo.

Akiy, 35, na mkewe wa miaka 36 walifika Wuhan, mji mkuu wa mkoa wa Hubei, kutoka Cameroon mnamo Mwaka 2009 na kuanza kufanya kazi ya kufundisha Kiingereza katika shule ya chekechea.

Tarehe 28 Septemba, mwaka 2021, mtoto wao Aubrey, akiwa katika hali mbaya ya kiafya alipelekwa kwenye idara ya uangalizi maalum wa wagonjwa katika hospitali hiyo ya Wuhan.

Mama yake na Aubrey, ambaye anaweza kuzungumza kiasi lugha ya Kichina, aliwaambia madaktari kuwa mtoto huyo alikuwa na homa kwa wiki mbili na hali yake haikua nzuri baada ya matibabu ya wiki moja katika hospitali karibu na nyumbani kwao.

Daktari Deng aliitwa kwa kutoa mashauriano juu ya mtoto. Madaktari waligundua Aubrey alikuwa na tatizo la kichwamaji pamoja na mkusanyiko mdogo wa damu chini ya dura mata, ambayo yalihitaji upasuaji wa dharura.

"Upasuaji umefanikiwa," Deng alisema. "Baada ya matibabu kadhaa ya kuzuia uambukizo, mtoto alikuwa nje ya hatarini na hali yake ilianza kupona."

Baada ya upasuaji huo, Deng na wenzake walikuwa karibu na Aubrey na wazazi wake. Alitembelea wodi yake kila siku kupata maendeleo ya afya ya mtoto huyo.

Baada ya upasuaji huo uliookoa uhai wa mtoto, wanandoa hao waliagiza bango maalum, lililotumwa kwa wafanyakazi wa afya wa idara ya uangalizi maalum wa wagonjwa ya hospitali hiyo kutoa shukrani zao. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha