China na nchi za BRI zanufaika na matunda ya ushirikiano wa kilimo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 01, 2021
China na nchi za BRI zanufaika na matunda ya ushirikiano wa kilimo
Picha ikionesha jengo ndani ya Ukanda wa Maendeleo ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Sudan. (Picha kutoka tovuti ya Shirikisho la Viwanda na Biashara la Taifa la China)

Katika miaka minane iliyopita tangu China itoe Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja (BRI), nchi hiyo imefanya jitihada za kuendelea kukuza ushirikiano wa kivitendo na nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo hilo katika sekta ya kilimo, sekta ambayo imepewa kipaumbele katika ushirikiano wa BRI, na kufikia maendeleo ya pande zote na ya pamoja na nchi husika.

Hadi sasa, China imetia saini makubaliano ya ushirikiano wa kilimo na nchi 86 za BRI na kuanzisha mifumo thabiti ya kufanya kazi na zaidi ya nusu ya nchi hizo. Katika miaka minane iliyopita, China imewekeza zaidi ya miradi 820 ya kilimo katika nchi za BRI.

Uwekezaji wa China katika nchi za BRI umezidi dola za kimarekani bilioni 17. Hadi kufikia mwaka jana wa 2020, thamani ya jumla ya biashara ya bidhaa za kilimo kati ya China na nchi zinazoshiriki katika BRI ilifikia dola za kimarekani bilioni 95.79.

Mwaka 2012, Kampuni ya Shandong International Economic & Technical Cooperation (CSI) na Kampuni ya Lumian, zote zikiwa na makao makuu katika Mji wa Jinan, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shandong Mashariki mwa China, kwa pamoja zilisajili kampuni mpya iitwayo New Epoch, Kampuni ya Maendeleo ya Kilimo nchini Sudan kwa ajili ya ujenzi wa Eneo la Maendeleo ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Sudan.

Awamu ya kwanza ya mradi inahusu uwekezaji uliopangwa wa thamani ya jumla ya dola za Marekani milioni 50, ambapo dola milioni 46 zimekwishapatikana na kuwekezwa.

Mwaka 2017, Eneo la Maendeleo ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Sudan lilitambuliwa kuwa moja ya sehemu za maeneo 10 ya kwanza ya kielelezo ya ushirikiano wa nje ya nchi wa kilimo na Wizara ya Kilimo na Masuala ya Vijijini ya China.

Kupitia njia hiyo ya kunufaishana, ukanda huo wa ushirikiano wa kilimo umeleta maendeleo ya kilimo katika eneo lote la umwagiliaji la Rahad nchini Sudan lenye ukubwa wa ekari milioni 2.2 (kama hekta 146,670).

Mwezi Septemba, Mwaka 2016, Kampuni ya mpira ya Guangken ya Guangdong, yenye makao yake makuu katika Mkoa wa Guangdong nchini China, ilichukua umiliki wa hisa za Kampuni ya mpira ya Thai Hua ya Thailand, ambayo ilikuwa ya tatu duniani kwa uzalishaji wa mazao ya mpira. Umiliki huu umeifanya kampuni hiyo kuwa moja ya kampuni kubwa zaidi duniani ya mazao ya mpira ambayo inamiliki mnyororo mzima wa uzalishaji wa mazao ya mpira asilia.

Kampuni hiyo ya China imezindua miradi 42 ya uzalishaji wa mpira wa asili katika nchi kama vile Thailand, Malaysia, Indonesia, Cambodia, Laos, na Singapore, na kujenga mfumo wa maendeleo wenye mnyororo kamili wa uzalishaji wa mpira ikiwa ni pamoja na utafiti, upandaji wa miche, usimamizi wa mashamba, usindikaji wa kina, uhifadhi na usambazaji na biashara ya kimataifa.

Katika mwaka huu wa 2021, Kampuni hiyo imezalisha na kuuza zaidi ya tani 700,000 za bidhaa kavu za mpira kutoka kwa miradi yake katika nchi mbalimbali. Pia imefungua viwanda 26 vya usindikaji wa mpira asilia nchini Thailand, Malaysia, na Indonesia vyenye uwezo wa kuzalisha jumla ya tani milioni 1.3 za mpira. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha