Tanzania katika maandalizi ya mwisho ya kuanzisha magari ya kusafiri angani kwa nyaya kwenye Mlima Kilimanjaro

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 01, 2021

DAR ES SALAAM – Bodi ya Utalii ya Tanzania imesema kuwa iko katika maandalizi ya mwisho ya kuanzisha magari ya kusafiri angani kwenye nyaya katika Mlima Kilimanjaro, mlima ambao ni mrefu zaidi barani Afrika.

Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amesema mchakato wa kuanzisha magari hayo unaendelea vema na utaanza hivi karibuni.

Masanja amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumanne ya wiki hii mjini Dodoma, Mji Mkuu wa Tanzania kuwa magari hayo yatatumiwa zaidi na watalii na watu wengine ambao hawawezi kutembea hadi kilele cha mlima kwa miguu.

Mlima Kilimanjaro, mojawapo ya vivutio vya utalii nchini Tanzania, una urefu wa mita 5,895 juu ya usawa wa bahari, huku takriban watalii 50,000 kutoka sehemu mbalimbali za Dunia wakijaribu kufika kilele cha mlima huo kila mwaka.

Mwezi Desemba, Mwaka 2020, Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) Paul Banga, alisema Serikali ya Tanzania imeidhinisha mradi wa magari ya kusafiri angani kwenye nyaya katika Mlima Kilimanjaro.

Banga alisema Serikali ilikuwa tayari imeipa TANAPA idhini ya kuwekeza kwenye mradi huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha