Je, ni hatua gani mpya za kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 01, 2021

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametangaza hatua mbalimbali za kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika wakati alipohutubia Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kupitia njia ya video siku ya Jumatatu ya wiki hii.

Yafuatayo ni mambo muhimu ya hatua hizo:

Mpango wa Matibabu na Afya

China itatoa dozi nyingine bilioni 1 za chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa Afrika ili kusaidia kutimiza lengo la kuchanja asilimia 60 ya watu wa Afrika ifikapo Mwaka 2022 la Umoja wa Afrika.

China itatekeleza miradi 10 ya matibabu na afya katika nchi za Afrika, na kutuma wataalamu wa afya ya umma na wataalam wa tiba 1,500 barani Afrika.

Kupunguza umaskini na kuendeleza kilimo

China itatekeleza miradi 10 ya kupunguza umaskini na kuendeleza kilimo na kutuma wataalam 500 wa kilimo barani Afrika.

China itaunga mkono Ushirikiano wa Kampuni za China barani Afrika kwa Majukumu ya Kibishara kwa Jamii katika kuzindua mpango wa "Kampuni 100 katika Vijiji 1,000."

Kuhimiza Biashara

China itaongeza zaidi bidhaa zisizo tozwa ushuru kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China, ili thamani ya jumla ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Afrika kufikia dola za Marekani bilioni 300 katika miaka mitatu ijayo.

China itatoa dola za kimarekani bilioni 10 kuunga mkono uuzaji bidhaa za Afrika kwa nchi za nje.

China itatekeleza miradi 10 ya mawasiliano barani Afrika.

Kukuza Uwekezaji

China itahimiza kampuni zake kuwekeza dola za kimarekani zisizopungua bilioni 10 barani Afrika katika miaka mitatu ijayo.

China itatekeleza miradi 10 ya kukuza viwanda na kuongeza ajira kwa Afrika, kutoa mikopo ya dola za kimarekani bilioni 10 kwa mashirika ya fedha ya Afrika, kupewa kipaumbele katika kusaidia maendeleo ya biashara ndogo na za kati za Afrika, na kuanzisha kituo cha kuvuka mpaka cha sarafu ya yuan ya China kati ya China na Afrika.

Uvumbuzi wa Kidijitali

China itatekeleza miradi 10 ya uchumi wa kidijitali barani Afrika, kuanzisha vituo vya ushirikiano kati ya China na Afrika kuhusu matumizi ya satelaiti za kuhisi kutoka mbali, na kuunga mkono ujenzi wa maabara ya pamoja ya China na Afrika, taasisi washirika, na vituo vya ushirikiano wa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia.

Maendeleo yasiyochafua mazingira

China itatekeleza miradi 10 ya maendeleo yasiyochafua mazingira, ulinzi wa mazingira na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa Afrika, kuunga mkono maendeleo ya "Ukuta Mkuu wa Kijani", na kujenga barani Afrika vituo vya maendeleo yanayotoa kaboni chache na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kujenga Uwezo

China itasaidia kujenga au kukarabati shule 10 barani Afrika, na kualika wataalamu 10,000 wa ngazi ya juu kutoka nchi za Afrika kwenye semina na warsha.

China itahimiza kampuni za China barani Afrika kutoa nafasi za ajira zisizopungua 800,000 kwa wenyeji. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha