China na Benin zakubaliana kusukuma mbele uhusiano katika hadhi mpya ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 03, 2021

DAKAR - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Benin Aurelien Agbenonci wamekubaliana kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili hadi kufikia hadhi mpya ya juu.

Wang na Agbenonci wamekutana mjini Dakar, Mji Mkuu wa Senegal, Jumanne ya wiki hii pembezoni mwa Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliomalizika mapema wiki hii.

Wang amesema uhusiano kati ya China na Benin umeimarika kwa kasi chini ya uangalizi na uongozi wa wakuu wa nchi hizo mbili, huku kukiwa na maendeleo endelevu ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali.

Aliongeza kwamba, China na Benin zimesaidiana na kuungana mkono katika kukabiliana na janga la UVIKO-19, na kuimarisha zaidi urafiki.

Aidha Wang amesema kuwa, China inathamini uungaji mkono wa Benin kwa China katika masuala yanayohusu maslahi yake ya kimsingi na mambo yanayohusu masuala yake makuu na itaendelea kuiunga mkono kwa dhati Benin katika kupinga kuingiliwa kati na nchi za nje na kuchagua njia yake ya kujipatia maendeleo na kwamba China iko tayari kushirikiana na Benin katika kuimarisha kwa kina uhusiano katika nyanja mbalimbali na kujitahidi kupata mafanikio mapya katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Agbenonci alisema kwamba, hotuba muhimu ya Rais Xi Jinping wa China kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC ni ya kutia moyo na siyo tu itainua kiwango cha ushirikiano kati ya Afrika na China bali pia italeta msukumo mpya kwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Amebainisha kwamba, Benin inashikilia kanuni ya “Kuwepo kwa China Moja” na kwamba itaendelea kuunga mkono kwa dhati msimamo wa haki wa China.

Pande zote mbili zilikubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili hadi kufikia hadhi mpya ya juu katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mwaka ujao. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha