“Baraza la Kimataifa la Congdu 2021” lafunguliwa Guangzhou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2021

"Baraza la Kimataifa la Congdu 2021" lilifunguliwa kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Congdu, Guangzhou Jumapili ya wiki iliyopita. Makamu wa rais wa China Wang Qishan alihudhuria ufunguzi akitoa hotuba.

Wang alisema, hivi sasa Dunia iko kwenye njiapanda mpya, jumuiya ya kimataifa inahitaji zaidi kuliko wakati wowote uliopita kuwa na maoni ya pamoja na nia thabiti, na kuhimiza maendeleo kwa pamoja.

Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya CPC ya Mkoa wa Guangdong Li Xi alihudhuria ufunguzi huo.

Watu zaidi ya 150 walihudhuria kwenye mkutano wa baraza hilo kwa njia ya video au kwenye ukumbi wa mkutano, wakiwemo baadhi ya viongozi wastaafu wa nchi mbalimbali, wakuu wa awamu zilizopita wa mashirika mbalimbali ya kimataifa, mabalozi wa nchi mbalibali walioko China na maofisa wa kidiplomasia wa nchi husika, wajumbe wa mashiriki wa kimataifa yaliyoko China, watu wa sekta za viwanda na biashara wa nchini na nje pamoja na wataalam na wasomi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha