Wataalam wasema Demokrasia ya China inawahakikishia watu wote haki ya maisha yenye furaha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2021
Wataalam wasema Demokrasia ya China inawahakikishia watu wote haki ya maisha yenye furaha
Picha ikionesha matoleo ya Lugha za Kichina na Kiingereza ya Waraka wenye kichwa cha "China: Demokrasia Inayofanya Kazi" katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali ya China mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Desemba 4, 2021. (Xinhua/Li He)

BEIJING - Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali ya China mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa waraka wenye kichwa cha "China: Demokrasia Inayofanya Kazi," ambao ulifafanua juu ya maadili, historia, mifumo ya kitaasisi, mazoea, na mafanikio ya demokrasia ya China.

Kwa mujibu wa wataalam na watafiti kutoka nchi mbalimbali duniani waliofanyiwa mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua, Demokrasia ya China imehakikisha haki ya watu wote ya kuwa na maisha yenye furaha na kuhimiza maendeleo ya haraka ya nchi.

"Mfumo wa kidemokrasia wa China unazingatia zaidi kama watu wana haki ya kutawala nchi yao, kama unakidhi mahitaji ya watu, na kama watu wana hisia ya kuridhika na furaha," Kin Phea, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa, katika Chuo cha Kifalme cha Cambodia amenukuliwa katika mahojiano na Xinhua.

"Ndiyo maana inapata uungwaji mkono mkubwa wa watu wa China kutoka nyanja zote za maisha," amesema.

Kwa upande wake Hamed Vafaei, Mkurugenzi wa Kituo cha Elimu ya Asia katika Chuo Kikuu cha Tehran, amesema kuwa hakuna demokrasia ya kiwango kimoja duniani, na kwamba watu katika kila nchi wanapaswa kutafuta mfumo wao wenyewe wa maendeleo na demokrasia.

Vafaei amebainisha kwamba, watu wa China wamechagua njia yao wenyewe, na maendeleo ya China katika nyanja mbalimbali, pamoja na mafanikio katika kupunguza umaskini, yote yamedhihirisha ubora wa juu wa demokrasia ya China.

Naye Bambang Suryono, Mwenyekiti wa Kituo cha Elimu ya Uvumbuzi cha Asia ambayo ni taasisi ya washauri mabingwa ya Indonesia, amesema kuwa demokrasia nzuri ni ile ambayo imejengwa kulingana na hali halisi ya nchi na ambayo pia inafanya kazi kwa manufaa ya watu.

Huku akidhihirisha kuwa demokrasia ya China inahudumia watu wake, Suryono ameongeza kwamba, demokrasia ya China imepata mafanikio makubwa katika kupunguza umaskini, huduma za afya, elimu na maeneo mengine.

Katika mahojiano yake, Mehmet Enes Beser, Mkurugenzi wa Kituo cha Bosphorus cha Elimu ya Asia nchini Uturuki, amesisitiza kwamba China daima imekuwa ikitoa kipaumbele kwa maisha ya watu wakati wa janga la UVIKO-19, akionesha kwamba demokrasia ya China imetekelezwa vizuri.

Ameongeza kwamba, kwa upande wa nchi nyingine za Magharibi, zilishindwa kuchukua hatua madhubuti na kwa wakati kipindi janga hilo lilipozuka, ikionesha kuwa "demokrasia" ilikuwa maneno matupu tu kwao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha