Marekani inaharibu demokrasia duniani kote: SCMP

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2021
Marekani inaharibu demokrasia duniani kote: SCMP
Mwandamanaji akiingia ndani ya Jengo la Bunge la Marekani. Picha imechukuliwa kwenye video iliyorushwa na Kituo cha Televisheni cha NBC huko Arlington, Virginia, Marekani, Januari 6, 2021. (Xinhua/Liu Jie)

HONG KONG – Makala yaliyochapishwa na Gazeti la South China Morning Post (SCMP) yanaeleza kwamba Marekani inaharibu demokrasia ndani na nje ya nchi hiyo na kwamba mkutano ujao wa kilele wa demokrasia ni dalili ya kile ambacho kinaonesha kasoro kubwa katika demokrasia ya Marekani.

Makala hiyo yenye kichwa cha "Mgonjwa wa demokrasia anaandaa mkutano wa kilele wa demokrasia" inaeleza kwamba, ikiwa kweli maendeleo ya demokrasia duniani yanarudi nyuma, Marekani inawajibika zaidi kwa hilo, na demokrasia yenyewe inarudi nyuma nchini Marekani hivyo nchi hiyo siyo mfano kwa nchi nyingine yeyote.

"Idadi kubwa ya washirika wa Marekani na nchi za muungano hazijashuhudia uboreshaji wa kidemokrasia katika muongo mmoja uliopita, ingawa nchi nyingi zisizo washirika wa Marekani zilifanya hivyo," makala hiyo inasema, ikibainisha kwamba mkutano huo "unaonekana zaidi kama genge."

Makala hiyo inabainisha kwamba, Marekani imeshuhudia polisi wake wakitumia nguvu kubwa na silaha za kijeshi, mfumo mbovu na wa kikatili wa magereza, ubaguzi wa kimfumo, na kunyimwa haki kwa makundi ya watu wachache, hasa watu weusi. "Haki za kupiga kura zimepunguzwa na mahakama zimetiwa siasa na majaji walioteuliwa, kutoka mahakama za chini hadi Mahakama ya Juu."

Imeeleza kwamba, kama demokrasia inahitaji kuboreshwa au kuungwa mkono kuna kazi nyingi za kufanywa ndani ya Marekani badala ya nje ya Marekani.

" 'Demokrasia' imekuwa mbinu ya ujanja ya Marekani kuendeleza na kudumisha umwamba wake wa duniani," inasema makala ya SCMP.

Marekani imealika nchi kadhaa kwenye mkutano huo uliopewa jina la "Mkutano wa kilele wa Demokrasia", zikiwemo washirika wake wakuu wa Magharibi. Mkutano huo uliotangazwa kwa muda mrefu utafanyika mtandaoni Tarehe 9 na 10 Desemba mwaka huu kabla ya mkutano wa ana kwa ana katika mkutano wake wa pili mwaka ujao. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha