Mji Mkuu Mpya wa Misri Waonesha Tamaa ya Ujenzi wa Mambo ya Kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2021
Mji Mkuu Mpya wa Misri Waonesha Tamaa ya Ujenzi wa Mambo ya Kisasa
Hili ni jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje lililoko Mji Mkuu mpya wa kiutawala wa Misri. Picha ilipigwa Novemba 3 na mwandishi wa habari wa Xinhua.

Ikulu ya Misri imetoa taarifa ikisema kuwa, kuanzia mwezi huu Serikali ya Misri imeanza kuhamia rasmi kwenye Mji Mkuu mpya wa kiutawala ulioko umbali wa kilomita 45 Mashariki mwa Mji wa Cairo katika eneo la jangwa. Mji Mkuu huo mpya na utafanya uendeshaji wa majaribio kwa miezi sita

Mji Mkuu huo mpya wa kiutawala ni moja ya jitihada mpya za “kujenga mji mpya kwenye jangwa” tokea miaka ya 1970. Mji huo una matarajio kadhaa kama vile kupunguza shinikizo la idadi ya watu katika Mji Mkuu wa Cairo, kuongeza nafasi za ajira, kuvutia uwekezaji wa nchi za nje na pia kuonesha tamaa ya Misri ya kuelekea maendeleo ya kisasa kwa taifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha