CPC yafanya mkutano kuhusu kazi za uchumi za 2022, kupambana na ufisadi, na kuweka kanuni za ukaguzi wa nidhamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2021

BEIJING - Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano uliohusu kuchambua na kusoma kazi za kiuchumi za Mwaka 2022, kupanga mienendo ya Chama na kazi ya kupambana na ufisadi, na kuweka kanuni zinazohusu ukaguzi wa nidhamu ya CPC.

Mkutano huo uliofanyika Jumatatu ya wiki hii umeendeshwa na Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.

Mkutano huo umeeleza kwamba, Mwaka 2021 umekuwa muhimu kwa Chama na Taifa. Umetaja mwitikio wa utulivu na ufanisi wa China kwa mabadiliko ya kimataifa na Janga la Virusi vya Corona ambalo halijapata kuonekana katika karne moja, kukamilika kwa kazi kubwa ya mageuzi na maendeleo na kupata mwanzo mzuri wa Mpango wa 14 wa Miaka Mitano ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii.

Mkutano huo umetaka kazi za kiuchumi zifanyike kwa njia thabiti chini ya mwongozo wa Mawazo ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya, wakati wa kuboresha maisha ya watu, kunatakiwa kukabiliana na UVIKO-19 na kuratibiwa na maendeleo ya uwiano ya kiuchumi.

Mkutano huo umebainisha kwamba, hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda uthabiti wa uchumi mkuu, kuweka viashirio vikuu vya kiuchumi ndani ya safu ifaayo na kudumisha utulivu wa kijamii ili kujiandaa kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

Pamoja na mambo mengine yaliyosisitizwa ikiwemo uthabiti wa sera za kifedha, mkutano huo umesisitiza kwamba sera ya kimuundo inapaswa kulenga kulainisha mzunguko wa uchumi wa kitaifa, kuboresha ushindani wa kimsingi wa viwanda na kuimarisha uthabiti wa mnyororo wa ugavi.

Mkutano huo umeeleza zaidi kwamba, juhudi zinapaswa kufanywa kuendeleza ujenzi wa nyumba za bei nafuu, kusaidia soko la nyumba za kibiashara ili kukidhi vyema mahitaji ya wanunuzi wa nyumba, na kuimarisha maendeleo himilivu na mzunguko mzuri wa sekta ya mali isiyohamishika, Pia umeeleza kwamba, sera za mageuzi na kufungua mlango zinapaswa kuimarisha msukumo wa maendeleo ya nchi,

Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu (CCDI) na Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi (BMT), pamoja na kamati za ukaguzi wa nidhamu na vyombo vya usimamizi katika ngazi zote zimetekeleza kwa uaminifu majukumu yaliyowekwa na Katiba ya CPC na Katiba ya nchi, kutoa hakikisho thabiti kwa mwanzo mzuri wa Mpango wa 14 wa Miaka Mitano ya Maendeleo ya Uchumi na Jami.

Mktuno huo umesema, vyombo vya ukaguzi na usimamizi wa nidhamu vimesisitizwa kubaki na nia ya kuboresha mwenendo wa Chama, kudumisha uadilifu na kupambana na rushwa, kujitahidi kufanya uboreshaji wa kitaasisi na mafanikio katika utawala, na kukuza shughuli za ukaguzi na usimamizi wa nidhamu zinazodhibitiwa vema kwa mujibu wa sheria.

Mkutano huo pia ulipitia Kanuni za Kazi za Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, ambazo zinaweka masharti ya kina kuhusu muundo wa uongozi, uendeshaji na majukumu ya kamati ya ukaguzi wa nidhamu ya Chama katika ngazi zote.

Kabla ya mkutano wa Jumatatu, Xi alikuwa ameendesha mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, ambapo Kamati Kuu ya ukaguzi wa nidhamu na Kamati ya Usalama wa Taifa ziliripoti kazi zao za Mwaka 2021 na maandalizi ya Kikao cha Sita cha Kamati kuu ya 19 cha ukaguzi wa nidhamu, ambacho kinatarajiwa kufanyika kuanzia Januari 18 hadi 20 Mwaka 2022. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha