Ufaransa yatoa stempu kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 24, 2022
Ufaransa yatoa stempu kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Msanii wa China anayeishi Paris, Chen Jianghong akisaini kwenye stempu za ukumbusho wa Mwaka wa Chui milia zilizobuniwa naye kwenye hafla ya utoaji stempu huko Paris, Ufaransa Januari 22. Kampuni ya huduma ya posta ya Ufaransa, La Poste Jumamosi ya wiki iliyopita imetoa stempu za miaka miwili ya chuimilia kushereherekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China. Stempu za mwaka huu zimebuniwa na msanii wa China Chen Jianghong mwenye makazi yake Paris. (Xinhua/Gao Jing)

PARIS, Jan. 22 (Xinhua) -- Kampuni ya huduma ya posta ya Ufaransa La Poste Jumamosi ya wiki iliyopita ilitoa stempu mbili kusherehekea ujio wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa chui milia utakaoanza Februari mosi.

Ikiwa na picha ya chui milia aliyejilaza kwenye mandharinyuma nyekundu, Stempu moja inatumika kwa huduma ya posta nchini Ufaransa kwa thamani ya euro 1.16.

Stempu nyingine ikiwa na picha ya chui milia anayekodolea macho mbali kwenye mandharinyuma ya bluu, ina thamani ya euro 1.65 kwa huduma ya posta ya kimataifa.

Chen Jianghong, msanii kutoka China, mbunifu wa stempu hizo, alisema chui milia hao wawili wanawakilisha nguvu na matumaini. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha