Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wafanyika Senegal

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2022
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wafanyika Senegal

Senegal ilifanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Januari 23 na imechagua viongozi wa mikoa 43 na miji na wilaya 557 nchini kote.

Zoezi la kupiga kura lilianza saa mbili asubuhi ya Tarehe 23 ya saa za huko na kuisha saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo. Katika nchi ya Senegal, kuna wapiga kura zaidi ya milioni 6 na vituo 15066 vya kupigia kura. Ili kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa vizuri, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Senegal ilipeleka wasimamizi zaidi ya 22,000 katika vituo vya kupigia kura.

Katika kituo cha kupigia kura kilichoko Dakar, mji mkuu wa Senegal, waandishi wa habari walishuhudia wapiga kura wakipanga foleni kupiga kura kwa utulivu na utaratibu. Kwa mujibu wa ripoti, baadhi ya vituo viliongeza muda wa kupiga kura kwa kuwa wapiga kura katika baadhi ya maeneo walishindwa kukamilisha upigaji kura kwa muda uliopangwa.

Rais Macky Sall wa Senegal alipiga kura siku hiyo. Baada ya kupiga kura alisema kuwa wapiga kura wanapaswa kutumia haki zao za kiraia kwa njia ya amani na kudumisha utulivu wa nchi kwa hiari. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha