Rais wa Malawi avunja baraza la mawaziri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2022

LILONGWE - Rais wa Malawi Lazarus Chakwera Jumatatu jioni ametangaza kuvunja baraza lake la mawaziri huku kukiwa na uvumi kwamba viongozi wengi wa ngazi za juu wa kisiasa, mahakama na wengine wanahusika katika kesi ya ufisadi inayomhusisha mfanyabiashara wa Malawi anayeishi Uingereza, Zuneth Sattar, ambaye anachunguzwa na mashirika ya kupambana na ufisadi ya Malawi na Uingereza.

Hii imefuatia mazungumzo ya simu yaliyovuja kati ya Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Ufisadi ya Malawi (ACB), Martha Chizuma, na mpiga simu ambaye hakutambulika, ambapo mkuu huyo wa ACB alifichua baadhi ya taarifa nyeti kuhusu uchunguzi wa kesi hiyo.

Rais ametoa onyo kali kwa Chizuma kwa tabia yake katika mawasiliano hayo ya simu yaliliyovuja, ambayo ameelezea kuwa ni utovu wa nidhamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha