Upepo mkali waua wavuvi na kusomba boti 60 za wavuvi Zanzibar, Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2022

DAR ES SALAAM - Angalau mvuvi mmoja ameuawa, nyumba 190 zilifurika maji na boti 60 za watalii na wavuvi zilisombwa na mvua kubwa na upepo mkali huko Zanzibar nchini Tanzania

Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar (ZDMC) Makame Khatib amesema Jumanne wiki hii kwamba mvuvi huyo alifariki dunia katika Kijiji cha Uroa pwani kufuatia boti yake kupinduka baada ya kupigwa na upepo mkali katika Bahari ya Hindi.

Amesema mvua kubwa iliyonyesha pamoja na upepo mkali ilivikumba Visiwa vya Zanzibar katika Bahari ya Hindi siku ya Jumamosi na Jumapili wiki iliyopita.

Khatib amesema nyumba nyingi zilizojaa maji ziko katika maeneo hatarishi ambayo yamepigwa marufuku kwa ujenzi wa nyumba.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais anayeshughulikia mambo ya Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Khalid Salum Mohamed amewataka wananchi kuacha kujenga nyumba katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha