China na nchi za Asia ya Kati zajipanga kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2022
China na nchi za Asia ya Kati zajipanga kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja
Rais Xi Jinping wa China akiendesha mkutano wa kilele wa mtandaoni kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na nchi tano za Asia ya Kati na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Januari 25, 2022. Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Zhaparov, Rais wa Tajik Emomali Rahmon, Rais wa Turkmen Gurbanguly Berdymukhamedov na Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev walihudhuria mkutano huo. (Xinhua/Li Xiang)

BEIJING - China na nchi tano za Asia ya Kati Jumanne wiki hii zimeweka mikakati ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja iliyo karibu zaidi, wakati Rais wa China Xi Jinping alipoendesha mkutano wa kilele wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na nchi tano za Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan.

"Haijalishi jinsi mazingira ya kimataifa yanaweza kubadilika au jinsi maendeleo ya China yanavyoweza kukua, China daima itaendelea kuwa jirani mwema, mshirika mzuri, rafiki mzuri, na ndugu mzuri ambaye nchi za Asia ya Kati zinaweza kumwamini na kumtegemea," Xi amesema na kusisitiza kujitolea kwa China katika eneo hilo.

Uhusiano wa kuigwa

Akisifu maendeleo ya uhusiano kati ya China na Asia ya Kati katika miongo mitatu iliyopita kama "mfano mzuri wa kukuza aina mpya ya uhusiano wa kimataifa," Xi amedokeza kwamba ufunguo wa mafanikio ya ushirikiano huo ni kuheshimiana, ujirani mwema, mshikamano katika nyakati ngumu na kunufaishana.

Viongozi wa nchi tano za Asia ya Kati wamepongeza matokeo mazuri ya ushirikiano na China, wakisifu maendeleo ya uhusiano kati ya nchi za Asia ya Kati na China ambayo siyo tu kwamba yamehimiza maendeleo na ustawi wao, lakini pia kulinda ipasavyo amani na utulivu wa kikanda.

Pande zote mbili zimesema mkutano huo kama hatua muhimu ya maendeleo kati ya pande hizo mbili.

Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja iliyo karibu zaidi

"China iko tayari kushirikiana na nchi za Asia ya Kati ili kuendeleza kasi zaidi na kujitahidi bega kwa bega kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Asia ya Kati iliyo karibu zaidi," Xi amesema katika hotuba yake, pia akitoa baadhi ya mapendekezo kutimiza lengo hilo.

Alitangaza kuwa China itaendelea kutoa chanjo na vifaa vya kukabiliana na janga la UVIKO-19 kwa nchi za Asia ya Kati, na itaimarisha kuzalisha chanjo kwa pamoja na kuhamisha teknolojia kuhusiana na chanjo na dawa dhidi ya UVIKO-19.

Viongozi hao wa Asia ya Kati wamesema watashirikiana na China "pamoja kwa mustakabali wa pamoja," wakirejea kauli mbiu ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing ya 2022, na wamesema wanatazamia kwa hamu kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo wiki ijayo.

Ushirikiano wa hali ya juu

Kwa mujibu wa ripoti ya Januari 17 mwaka huu ya Wizara ya Biashara ya China, biashara kati ya China na nchi za Asia ya Kati imeongezeka kwa zaidi ya mara 100 katika miaka 30 iliyopita, na uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika nchi hizo tano zilizidi dola za kimarekani bilioni 14.

Wachambuzi wamesema, kutegemeana baina ya uchumi wa China na uchumi wa nchi hizo tano unatoa uwezekano mkubwa wa kupanua ushirikiano wao wa kivitendo.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo, China na nchi za Asia ya Kati zimekubaliana kuimarisha uunganishaji wa Pendekezo la “Ukanda Mmmoja, Njia Moja" na mikakati ya maendeleo ya nchi hizo tano.   

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha