Rais Biden amteua msemaji mpya wa Ikulu ya Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 06, 2022

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jen Psaki(kulia), akimsikiliza msemaji mpya Karine Jean-Pierre wakati wa mkutano na waandishi wa habari Mei 5, 2022. (Picha kutoka Chinanews)

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press, Tarehe 5 kwa saa za huko, Rais Joe Biden wa Marekani alitangaza kumteua naibu msemaji wa Ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre kuwa msemaji anayefuata wa Ikulu ya Marekani.

Habari zinasema kuwa, Karine Jean-Pierre atakuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyeteuliwa kuwa msemaji wa Ikulu ya Marekani, ataanza kazi rasmi badala ya msemaji wa sasa Psaki Tarehe 13, Mei.

Biden alisema katika taarifa yake kuwa, Karine Jean-Pierre analingana na matakwa ya kuwa msemaji kuhusu "uzoefu, uwezo na uadilifu", na pia Psaki alimsifu kuwa ni "mshirika mwenzi wa kweli."

Habari nyingine zinasema kuwa, Psaki atajiunga na MSNBC na kuwa mtangazaji wa vipindi vinavyorushwa kwa njia ya internet baada ya kuondoka Ikulu ya Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha