Balozi mpya wa China awasilisha Barua ya Utambulisho wa Kitaifa kwa Rais wa Zambia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2022

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui kwenye Ikulu ya Lusaka, Zambia, Mei 12, 2022. Du Xiaohui, Balozi mpya wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Zambia, amewasilisha Barua ya Utambulisho wa Kitaifa kwa Rais wa Zambia Hakainde Hichilema mjini Lusaka siku ya Alhamisi wiki hii. (Xinhua/Martin Mbangweta)

LUSAKA - Du Xiaohui, Balozi mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China katika Jamhuri ya Zambia, amewasilisha Barua ya Utambulisho wa Kitaifa kwa Rais wa Zambia Hakainde Hichilema huko Lusaka, mji mkuu wa Zambia siku ya Alhamisi wiki hii.

Baadaye pande mbili zlifanya mazungumzo marefu na ya kirafiki.

Balozi Du amesema kuwa ni heshima na wajibu mkubwa kutumwa Zambia.

Ameeleza kuwa, urafiki wa nyakati zote kati ya China na Zambia ulianzishwa na viongozi waanzilishi wa nchi hizo mbili. Na baadaye umeendelezwa kizazi hadi kizazi, na kukita mizizi mioyoni mwa watu wa pande zote mbili.

“Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi, China na Zambia siku zote zimefuata kanuni za kuheshimiana, kuwa na usawa na kunufaishana, kushughulikia maslahi ya msingi na masuala makuu ya kila mmoja wao, kuhimiza ushirikiano ili kuleta manufaa kwa watu wa nchi zetu mbili, na kulinda haki na usawa wa kimataifa, na maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea” Du amesema.

Kwa upande wake Rais Hichilema alisema kuwa Zambia na China zinafurahia urafiki wa muda mrefu na wenye uhusiano wa karibu wa maslahi na ushirikiano wa kunufaishana katika sekta za uchumi, utamaduni na usalama.

Aliishukuru China kwa msaada wake mkubwa katika kupambana na janga la virusi vya Korona na akaeleza nia yake ya kupata uzoefu wa maendeleo ya China na kufanya ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Hichilema alisema kuwa hakuna kikomo kwa ushirikiano kati ya Zambia na China. Kwamba Zambia itaendelea kudumisha uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili na urafiki baina ya watu wa pande mbili ili kuendelea kuimarisha zaidi msingi wa urafiki.

Kwa kuzingatia umuhimu mkubwa wa urafiki wa nyakati zote kati ya nchi hizo mbili, Jamhuri ya Zambia ilipanga hafla tofauti ya kutoa nishani kwa balozi wa China, ambapo ni mara ya kwanza tangu aingie madarakani kwa Rais Hichilema kushiriki kwenye hafla ya kutoa nishani kwa mjumbe maalum wa kigeni.

Hafla ilifana sana, ilijaa ukarimu na urafiki. Stanley Kakubo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Zambia na Maofisa wakuu wa Ubalozi wa China nchini Zambia pia walishiriki kwenye hafla hiyo.

Du aliwasili Zambia kuanza kazi Tarehe 17 Aprili 2022.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha