Umoja wa Ulaya watoa mpango wa uwekezaji wa Euro bilioni 300 ili kupunguza utegemezi wa nishati kwa Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2022
Umoja wa Ulaya watoa mpango wa uwekezaji wa Euro bilioni 300 ili kupunguza utegemezi wa nishati kwa Russia
Tarehe 18 Mei, Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya (EU) Ursula von der Leyen akitoa hotuba katika makao makuu ya Kamati ya Umoja wa Ulaya huko Brussels, Ubelgiji.

Tarehe 18 Kamati ya Umoja wa Ulaya ilitoa mpango wa uwekezaji wa jumla ya Euro bilioni 300 ikitaka kutekeleza hatua mbalimbali katika miaka kadhaa ijayo ili kupunguza utegemezi wa nishati ya visukuku ya Russia, na kutumia nafasi hii kuharakisha kuipelekea nchi hiyo kutumia nishati safi. Mpango huo unaitwa REPowerEU, maana yake ni "kutoa upya nishati kwa Umoja wa Ulaya". Siku hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya (EU) Ursula von der Leyen alitangaza mpango huo kabambe wa uwekezaji katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya huko Brussels, Ubelgiji. (Mpiga picha: Zheng Huansong/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha