Ukraine yaamua kuongeza muda wa hali ya kivita ya nchi hii kwa siku 90

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2022

Bunge la taifa la Ukraine lilitoa habari kwenye tovuti yake rasmi tarehe 18 kuhusu kuidhinisha rasimu ya amri ya rais ya kuongeza muda wa hali ya kivita ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa amri mpya ya rais, muda wa hali ya kivita ya Ukraine utaongezwa kwa siku 90 baada ya kufikia saa 5:30 ya Mei 25.

Shirika la Habari la Ukraine lilitoa Habari zikisema kuwa, Tarehe 24, Februari, Bunge la taifa la Ukraine lilipitisha amri ya rais ya utekelezaji wa hali ya kivita kwa siku 30 nchini Ukraine, tangu hapo, Bunge la taifa la Ukraine liliidhinisha mara mbii amri ya Rais ya kuongeza muda wa hali ya kivita ya nchi hiyo hadi Aprili 25 na Mei 25.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha