Jukwaa jipya la Kuhimiza biashara kati ya China na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2022

(Picha inatoka Chinadaily.)

Jukwaa jipya la kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika lilianzishwa hapa Beijing Jumanne wiki hii.

Kamati ya usimamizi wa eneo la uchumi la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Daxing wa Beijing ilisema, kituo cha ushirikiano wa uvumbuzi wa Asia na Afrika kimeanzishwa kwa kufuata pendekezo la rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) lililohusu kuanzisha kituo cha ushirikiano wa uvumbuzi wa China na Afrika, ili kuhimiza uvumbuzi na ujasiriamali wa vijana wa China na Afrika.

Kituo hicho kimeanzishwa na kamati hiyo ya usimamizi, ofisi za ubalozi wa nchi mbalimbali za Afrika nchini China, pamoja na kampuni za China ikiwemo Kampuni ya Biashara ya kimataifa ya Njia ya Hariri ya Asia na Afrika.

Kamati hiyo ilisema, itakuwa njia muhimu kwa wafanyabiashara wa China na Afrika kufanya biashara kwa ufanisi zaidi. Itaimarisha ushirikiano na nchi za Afrika, kuboresha mazingira na huduma za biashara. Na kituo hicho kitahimiza ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya biashara, uwekezaji, teknolojia, uhifadhi wa mazingira, utamaduni, utalii na elimu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha