Waziri Mkuu wa China ahimiza juhudi za kuleta utulivu wa ajira, kulinda shughuli za watu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2022
Waziri Mkuu wa China ahimiza juhudi za kuleta utulivu wa ajira, kulinda shughuli za watu
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akiongoza kongamano wakati wa ziara ya kukagua Wizara ya Mambo ya Kiraia na Wizara ya Rasilimali Watu na Uhakikisho wa Kijamii, Juni 27, 2022. (Xinhua/Liu Weibing)

BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang ametoa wito kwa juhudi kubwa zaidi za kuharakisha ufufuaji wa uchumi ili kuimarisha soko, kuhakikisha utulivu wa ajira na kulinda shughuli za watu.

Li, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ameyasema hayo Jumatatu wiki hii alipofanya ziara ya kukagua wizara mbili za serikali ya China.

Akiwa katika ziara ya kutembelea kituo cha uelekezi wa kiufundi na utoaji wa mafunzo ya ajira cha Wizara ya Rasilimali Watu na Uhakikisho wa Kijamii, Li amehimiza juhudi za kuhamasisha watu wengi kufanya ujasiriamali, kufanya uvumbuzi, na kutoa msaada sawa kwa wadau wa soko wa aina zote, wakiwemo wale wa sekta binafsi na watu walioanzisha shughuli zao.

Mafunzo ya ufundi stadi lazima yaendane na mahitaji ya soko, Li amesema, akisisitiza umuhimu wa kutumia ipasavyo nguvu bora ya China katika rasilimali watu.

Baada ya kusikiliza ripoti kuhusu hali ya sasa ya ajira nchini China, Li amesema kuwa ajira imara ni ishara muhimu ya kuonesha viwango vinavyofaa vya uendeshaji wa uchumi. Uchumi wa China umepiga hatua katika kuimarika, lakini mambo ya msingi ya kufufua bado hayajaimarika vya kutosha na kazi za kuleta utulivu wa ajira bado ni ngumu.

Li amesisitiza utekelezaji zaidi wa sera zote ili kurudisha uchumi kwenye hali ya kawaida haraka iwezekanavyo.

Katika ziara yake kwenye Wizara ya Mambo ya Kiraia, Waziri Mkuu alikagua hali ya kufuatilia watu wa kipato cha chini na utekelezaji wa sera za usaidizi wa kijamii. Ametoa wito kwa juhudi za kuratibu sera za usaidizi wa kijamii na sera za ajira na kuhimiza watu kufanya kazi kwa bidii ili kupata maisha bora.

Li amesema kuwa kutokana na athari ya maambukizi ya virusi vya korona na maafa ya kimaumbile kumesababisha ongezeko la idadi ya watu wanaokabiliwa na changamoto. Amesisitiza kuimarisha kazi ya kuwafuatilia kwa wakati watu wanaohitaji msaada katika mifumo ya usaidizi wa kijamii, kupanua kiwango cha usaidizi wa kijamii na misaada, na kuzuia idadi kubwa ya watu wa China walioondokana na umaskini wasirudi nyuma kwa wingi kwenye umaskini tena.

“Juhudi pia zinapaswa kufanywa ili kuhakikisha kuwa pensheni zinalipwa kwa ukamilifu na kwa wakati, na kazi ya serikali kuhusu elimu ya lazima na huduma ya msingi ya afya na makazi lazima ifanywe vyema,” Li amesema.

Ameongeza kuwa Serikali katika ngazi zote zinahitaji kutekeleza unyumbulifu wa kibajeti na kubeba majukumu yao kwa ajili ya kulinda shughuli za kimsingi za watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha