China yaonya matokeo mabaya ya uwezekano wa ziara ya Spika wa Bunge la Marekani Pelosi kwenye eneo la Taiwan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2022

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Zhao Lijian Jumatatu wiki hii alisema kuwa upande wa China utachukua hatua za uthabiti na zenye nguvu kwa kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya China kama Marekani itahimiza uwezekano wa ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi kwenye eneo la China la Taiwan.

"Upande wa China umerudia kueleza wazi kwa upande wa Marekani ufuatiliaji wetu wa makini juu ya uwezekano wa ziara ya Pelosi katika eneo la Taiwan na upinzani wetu thabiti kwa ziara hiyo," Zhao amewaambia waandishi wa habari kwenye mkutano wa kila siku na wanahabari.

"Tuko tayari kikamilifu kwa tukio lolote," amesema.

"Marekani lazima iwajibike kikamilifu kwa matokeo yoyote makubwa yatakayotokea," Zhao ameongeza.

Mwezi Aprili mwaka huu spika huyo wa Bunge la Marekani alipanga kuzuru eneo la Taiwan, kitendo ambacho kilipingwa na kulaaniwa vikali na Balozi wa China nchini Marekani Qin Gang. Katika taarifa yake Qing aliitaka Marekani kufuta mara moja ziara hiyo.

Hata hivyo, ziara hiyo ya Pelosi iliahirishwa mwezi huo wa Aprili baada ya kiongozi huyo wa Bunge la Marekani kukutwa na maambukizi ya virusi vya Korona siku chache kabla ya siku ya ziara hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha