Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amteua Li Junhua wa China kuwa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya kiuchumi na kijamii

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2022

Balozi wa China nchini Italia Li Junhua (Kulia) akimkabidhi cheti Juan Lucas Restrepo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Anuwai ya Viumbe na Kituo cha Kimataifa cha Kilimo cha Kitropiki (CIAT), kwenye Ubalozi wa China nchini Italia huko Rome, Italia, Mei 31, 2022. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatatu wiki hii amemteua Li Junhua wa China kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kiuchumi na kijamii. (Xinhua/Jin Mamengni)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatatu wiki hii amemteua Li Junhua wa China kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kiuchumi na kijamii.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inasema, Li ambaye kwa sasa ni Balozi wa China nchini Italia na San Marino, atakuwa kazini badala ya Bw.Liu Zhenmin wa China, ambaye Guterres amemshukuru kwa kujituma kwa bidii na utumishi wake wa kujitolea kwa chombo hicho cha Dunia katika muda wake wa kazi utakaomalizika sasa hivi.

Li alizaliwa Mwaka 1962, alianza kazi yake katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mwaka 1985, na amehudumu katika nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa Balozi wa China nchini Myanmar, na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mashirika na Mikutano ya Kimataifa iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

Taarifa hiyo imesema Li ana shahada ya uzamili katika sera ya umma ya kimataifa aliyoipata kutoka Chuo cha utafiki wa maswala ya kimataifa wa Mafunzo ya Juu katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha