China yakanusha ripoti dhidi yake iliyotolewa na Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2022

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Zhao Lijian Jumatano wiki hii alikanusha ripoti ya Marekani dhidi ya China, akisema ni habari potofu za kisiasa zilizotungwa na Wabunge wachache wa Chama cha Republican na hazina msingi kabisa.

Zhao aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipotoa maoni yake kuhusu kile kinachoitwa ripoti iliyotolewa na wanachama wa chama cha Republican kwenye Kamati ya Baraza la Seneti inayoshughulikia masuala ya Usalama wa Ndani na ya Kiserikali ya Marekani. Hicho kinachoitwa ripoti kinasema kuwa wafanyakazi wa Benki Kuu ya Marekani walitoa mikataba ya kuajiri watu wenye vipaji kutoka China ambao baadaye waliwataka watoe taarifa za benki hiyo kuhusu uchumi wa Marekani, mabadiliko ya viwango vya riba na sera nyinginezo.

"Inaonekana kwamba baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanaweza kuwa na 'ugonjwa wa kuichukia China' au udanganyifu wa mateso na kuonyesha dalili mbaya kabisa. Tumeona kuwa Benki Kuu ya Marekani imetuma barua kwa wabunge husika, kuelezea mashaka na kutoridhika na maudhui ya ripoti," Zhao amesema. "Hii inasema mengi juu ya chanzo na lengo linalojulikana la ripoti hii."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha