Katibu Mkuu wa UM amuomba radhi rais wa DRC kwa ghasia zilizofanywa na walinda amani

(CRI Online) Agosti 02, 2022

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UM) Bw. Antonio Guterres amezungumza na Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa njia ya simu akimpa salamu zake za rambirambi na kumuomba radhi kwa tukio la Jumapili, ambapo walinda amani wa Umoja wa Mataifa walifyatua risasi na kuwaua wakazi wawili katika mji wa mpakani.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa umejitolea kikamilifu kwenye suala la amani, na kuratibiana na kufanya kazi na wanajeshi wa DRC, na kwamba mazungumzo yenye ufanisi yanahitajika ili kutatua hali hiyo na kuleta utulivu mashariki ya DRC. Pia amesisitiza haja ya kuanzisha uwajibikaji kwa matukio kama haya na kuridhia uamuzi wa mwakilishi wake maalum nchini DRC Bw. Bintou Keita, kuwashikilia walinda amani waliohusika na tukio hilo na kuanzisha uchunguzi mara moja.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha