Jeshi la China laanza mazoezi ya kijeshi karibu na Kisiwa cha Taiwan

(CRI Online) Agosti 03, 2022

Jeshi la Ukombozi wa Umma la China PLA la Kamandi ya Eneo la Vita la Mashariki limeanza mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya mfululizo karibu na kisiwa cha Taiwan jana usiku.

Mazoezi hayo ya pamoja ya mafunzo yanafanyika katika maeneo ya baharini karibu na pwani ya kaskazini, kusini magharibi na kusini mashariki mwa kisiwa hicho na anga zao, na pia mazoezi ya urushaji makombora ya masafa marefu yanafanyika katika Mlango Bahari wa Taiwan na majaribio ya kawaida ya makombora kwenye pwani ya mashariki ya kisiwa hicho.

Operesheni hizo za kijeshi ni hatua ya lazima kutokana na hivi karibuni kuongezeka kwa vitendo vibaya vya Marekani juu ya swala la Taiwan, na ni onyo kali dhidi ya shughuli za kuitaka “Taiwan ijitenge na China”.

Habari nyingine zinasema naibu waziri wa mambo ya nje wa China Xie Feng alimuita haraka balozi wa Marekani nchini China Nicholas Burns usiku wa kuamkia leo na kutoa malalamiko makubwa dhidi ya ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi katika kisiwa cha Taiwan, China. Akibainisha kuwa Pelosi anajiingiza kwenye hatari ya kulaaniwa na watu wote kwa kuchochea na kucheza na moto kwa makusudi, Xie alisema huu ni ukiukaji mkubwa wa kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha