Rais wa Marekani aidhinisha msaada mkubwa wa silaha kwa Ukraine

(CRI Online) Agosti 09, 2022

Rais wa Marekani Joe Biden jana alitangaza kuwa nchi hiyo itaipatia Ukraine msaada wa nyongeza wa usalama wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1, ikiwa ni silaha nyingi zaidi kutolewa kwa mara moja tangu kuanza kwa mgogoro kati ya Russia na Ukraine.

Tangu rais Biden aingie madarakani, msaada ulioahadiwa kutolewa na Marekani kwa usalama wa Ukraine umefikia dola za kimarekani bilioni 9.8 kwa jumla.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha