Rais wa Zambia ashiriki kwenye sherehe ya uzinduzi wa eneo la ukumbusho la Reli ya TAZARA

(CRI Online) Agosti 11, 2022
Rais wa Zambia ashiriki kwenye sherehe ya uzinduzi wa eneo la ukumbusho la Reli ya TAZARA
Picha iliyopigwa Juni 2, 2022 ikionesha makaburi ya wahandisi na wafanyakazi Wachina kwenye eneo la ukumbusho la Reli ya TAZARA huko Chongwe, Lusaka, Zambia. (Xinhua/Martin Mbangweta)

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema jana aliposhiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa eneo la ukumbusho wa Reli ya TAZARA amesema, serikali yake inafanya juhudi kustawisha reli ya TAZARA, ili kuifanya iwe njia muhimu ya usafirishaji kwa nje.

Rais Hichilema amesema, Zambia itafanya ushirikiano wa karibu na China na Tanzania, na kuongeza uwezo wa uendeshaji wa reli hiyo, ili iweze kuonesha umuhimu mkubwa zaidi katika usafirishaji wa mizigo na abiria.

Serikali ya Zambia inapanga kulifanya eneo la ukumbusho wa Reli ya TAZARA kuwa kivutio muhimu cha utalii, ili kueneza moyo wa Reli ya TAZARA na kustawisha shughuli za utalii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha