Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Afrika ya Kati chatuma kikosi cha dharura ili kuwalinda raia

(CRI Online) Agosti 11, 2022

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) kimetuma kikosi cha mwitikio wa haraka Jumatano ili kuwalinda raia katika Jimbo la Bamingui-Bangoran.

Dujarric amesema askari hao walipelekwa Ndele kutokana na taarifa za uwezekano wa kutokea mashambulizi ya makundi yenye silaha.

Jumatatu wiki hii, kutokana na msaada wa kikosi hicho, Mahakama Maalumu ya Jinai ilifungua tena kesi dhidi ya watu watatu wanaodaiwa kuwa wanachama wa Kundi la 3R. Kesi hiyo inahusisha mauaji ya takriban raia 40 huko Lemouna na Koundjili yaliyotokea mwezi Mei mwaka 2019.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha