Wasimamizi wa uchaguzi barani Afrika waipongeza Kenya kwa kufanya uchaguzi huru na wa haki

(CRI Online) Agosti 12, 2022

(Picha inatoka CFP.)

Mashirika ya kikanda barani Afrika yamesema uchaguzi mkuu uliofanyika jumanne wiki hii nchini Kenya ulikuwa wa utulivu, huru na wa haki.

Timu ya pamoja ya wasimamizi wa uchaguzi wa Kenya kutoka Umoja wa Afrika (AU) na Soko la Pamoja la Kusini na Mashariki mwa Afrika (COMESA), na tume ya usimamizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Shirika la Maendeleo ya Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) imesema katika taarifa zake kuwa, wameridhishwa na zoezi la uchaguzi, na kwamba kulikuwa hakuna upungufu mkubwa katika usimamizi wa usalama.

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya EAC Jakaya Kikwete amesema zoezi hilo liliendana na sheria za nchi na za kimataifa, na kuleta uaminifu kwa wapiga kura na wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa. Pia ameipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya kwa kuwekeza katika teknolojia mpya na kuwaandaa watu wenye ujuzi ili kuhakikisha uchaguzi wa viongozi wapya unakuwa jumuishi, wa wazi na wa uhakika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha