China na Sudan Kusini zaanza kutekeleza miradi muhimu chini ya FOCAC

(CRI Online) Agosti 12, 2022

Sudan Kusini itaanza kuvuna matunda ya Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana nchini Senegal.

Kaimu Balozi wa Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini Ma Wenjun amesema mjini Juba kuwa, nchi hizo mbili zitaanza kufanya utekelezaji wa pamoja wa miradi 9 itakayoendana na hali halisi ya nchi ya Sudan Kusini.

Alisema miradi hiyo ni pamoja na mradi wa dawa za Kichina ambao utashuhudia kuwasili kwa timu ya 10 ya matibabu ya China yenye madaktari 15 nchini Sudan Kusini mwezi Septemba. Mradi mwingine ni teknolojia ya upandaji wa nyasi za Juncao unaolenga kufundisha na kutangaza teknolojia ya kilimo cha Juncao kwa uzalishaji wa uyoga kwa ajili ya chakula na tiba, na upandaji wa majani hayo kwa ajili ya malisho ya mifugo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha