Rais Xi Jinping wa China akutana na Rais wa Azerbaijan, Aliyev

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2022
Rais Xi Jinping wa China akutana na Rais wa Azerbaijan, Aliyev
Mchana wa Septemba 15 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China alikutana na Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan katika Jumba la Wageni wa Taifa la Samarkand. (Mpiga picha: Zhai Jianlan/Xinhua)

Mchana wa Septemba 15 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China alikutana na Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan katika Jumba la Wageni wa Taifa la Samarkand.

Rais Xi Jinping alisema kuwa mwaka huu ni miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Azerbaijan. Upande wa China unaunga mkono njia za maendeleo zilizochaguliwa na watu wa Azerbaijan wenyewe. Pande hizi mbili zinatakiwa kutendea na kupanga uhusiano kati ya nchi hizi mbili kutoka mtazamo wa kimkakati, kuongeza zaidi hali ya kuaminiana kimkakati na kuungana mkono, kuendeleza kwa kina ushirikiano unaonufaishana kati ya pande hizi mbili, kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali uendelezwe kwa utulivu, kwa kina na kufuata hali halisi. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha